Jumapili 22 Machi 2026 - 18:00
Mapambano ya muqawama ni ahadi na wajibu wetu ambao hatutauacha

Hawza/ Abu Alaa al-Wala’i, Katibu Mkuu wa Kata’ib Sayyid al-Shuhada, huku akisisitiza kuendelea muqawama dhidi ya vitisho vinavyoikabili dini na taifa, alielezaa kuwa; dhana yoyote kuhusu kuiacha njia hii kuwa ni dhana batili.

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Katibu Mkuu wa Kata’ib Sayyid al-Shuhada (Muqawama wa Kiislamu wa Iraq), kupitia ujumbe alioutoa na kuchapishwa katika mtandao wa X, alisisitiza kwamba: Kupambana na vitisho dhidi ya dini na taifa ni ahadi thabiti na wajibu mtakatifu ambao hatutauacha kamwe.

Tarjama ya ujumbe wake ni kama ifuatavyo:

“Sisi ndani ya Kata’ib Sayyid al-Shuhada tunaamini kwamba; muqawama ni wajibu kama agano ambao hauwezi kuepukwa, na ni wajibu kama swala ambao hauwezi kupuuzwa. Na yeyote anayefikiri kwamba tutavunja agano letu au tutaacha swala, basi abebe pia dhana hiyo [batili] kwamba inawezekana tuache muqawama.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha